Muziki

Muziki

Darassa
Muziki by Darassa featuring Ben Pol, new Tanzanian rap song

Intro

Rudi utotoni 

Usipotembea utabebwa mgongoni

255 champion boy 

Niite Mbwana Samata

 

Verse 1

Wanaota mapembe waongezee mkia

Na Ukinibeep tunakupigia

And let me make one thing clear

Blah blah sitaki kusikia

Sio Simba sio Chui sio Mamba

Ngozi yangu inatosha kujigamba

Na sina maneno ya kwenye Khanga

Kazi juu ya kazi yani Bamba to bamba

Mzaa unawezaa kuzaa kizaazaa

Sinzia na fegi uchome kibanda

Kalale uote ndoto zako za kitanda

Sisi bado tupo macho mida ya wanga

Funga mkanda kaza na kamba

Ama ufate nyayo uchane msamba

Pasua miamba pasua anga

Tunasemaga chambua kama karanga

 

Chorus

Maisha na Muziki

Acha maneno weka muziki

Ukiwa sad ukiwa happy 

Ukiwa juu ukiwa chini

Piga muziki

yeah

Safari na muziki

yeah 

Acha maneno weka muziki

yeah

Imba unachopenda na ukitaka kucheza

Cheza Mziki

Bambata shika kamata

Rumba sakata

Nnapokaa mchizi nshadataa nshadataa

 

Verse 2

Unataka kukimbia na hauna break

What do you expect

Bongo, Congo au kwa Thabo Mbeki

Cheza lokasa ya mbongo uweze kumake

Watch yourself usije jiconfuse

Mzuka wa kuruka reggae kwenye blues

Una mchuzi no excuse

Maisha yetu kila siku kama vile kwenye movie

Vitu vingine havitakag ujuaji

Utajikuta unatandikia watu jamvi

Kusubiria embe chini mnazi

Kumwelewesha chizi utajipa kazi

Funga mkanda kaza na kamba

Ama ufate nyayo uchane msamba

Pasua miamba pasua anga

Tunasemaga chambua kama karanga

 

Chorus

Maisha na Muziki

Acha maneno weka muziki

Ukiwa sad ukiwa happy 

Ukiwa juu ukiwa chini

Piga muziki

yeah

Safari na muziki

yeah 

Acha maneno weka muziki

yeah

Imba unachopenda na ukitaka kucheza

Cheza Mziki

 

Hook

Wanatamani tupotee kwenye map

Tunapeleka game to the top top

I thought i told that we don't stop

Don't stop we don't stop

Wanatamani tupotee kwenye map

Tunapeleka game to the top top

I thought i told you that we don't stop

we don't stop